Young Africans Sports Club kujenga uwanja wa kisasa Jangwani

MBEYA-Rais wa klabu ya Yanga,Mhandisi Hersi Said amesema kuwa, mdhamini na mfadhili wa Klabu ya Yanga, Ghalib Said Mohammed (GSM) ameridhia kushiriki kufanikisha ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Young Africans Sports Club.
Dimba hilo litajengwa katika eneo la makao makuu ya klabu hiyo Jangwani jijini DarEes Salaam.

Ameyasema hayo Februari 11, 2024 mkoani Mbeya kwenye sherehe za miaka 89 za kuzaliwa kwa klabu hiyo kongwe nchini.

“Baada ya mazungumzo ya muda mrefu na mdhamini na mfadhili wa klabu yetu, Ghalib Said Mohammed (GSM), nipende kuwataarifu wanachama na mashabiki wa klabu yetu kuwa leo, GSM ameridhia kwa dhati kushiriki kwenye kufanikisha ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Young Africans Sports Club, katika eneo la makao makuu ya klabu yetu, Jangwani jijini Dar es Salaam.

“Nichukue fursa hii kumshukuru sana GSM kwa dhamira hiyo inayokwenda kutimiza ndoto ya uongozi wangu, Kamati ya Utendaji na wanachama na mashabiki wa Young Africans kwa kuwa na uwanja wetu.

“Kwa niaba ya uongozi, wanachama na nashabiki wa Young Africans SC, nipende kumuahidi GSM, kuwa tutampa ushirikiano wote utakaohitajika kuhakikisha tunafanikisha ujenzi wa uwanja wetu,"amesema Mhandisi Said.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news