Zanzibar kuanzisha Kitengo cha Magonjwa ya Moyo

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na Taasisi ya JKCI kwa kuanzisha kitengo cha kuhudumia magonjwa ya moyo Zanzibar katika Hospitali ya Mkoa Lumumba.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Februari 10,2024 wakati akifunga kongamano hilo la Wataalamu wa Kimataifa wa magonjwa ya moyo liloandaliwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI na Wizara ya Afya Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport lililowashirikisha Wataalamu wa Afya ndani na nje ya nchini.

Rais Dkt.Mwinyi amesema, Serikali itawekeza katika vifaa vyote vya matibabu ya Moyo Zanzibar.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameagiza Wizara ya Afya Zanzibar kuanza haraka majadiliano na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ili huduma za upasuaji wa moyo zianze kutolewa Zanzibar kipindi kifupi kijacho.

Rais Dkt. Mwinyi pia amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatenga rasilimali zilizopo ili kuendeleza juhudi za utafiti, kinga na matibabu ya magonjwa ya moyo.
Vilevile Rais Dkt. Mwinyi amesema, dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuimarisha huduma za Afya kwa kutoa matibabu ya magonjwa ya moyo na kupunguza vifo vinavyoweza kuepukika.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amewahimiza wananchi kutumia vyakula vinavyoshauriwa na wataalamu pamoja na kufanya mazoezi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news