Dkt.Mpango atoa maelekezo kwa wizara za Ardhi na Ulinzi

NA MUNIR SHEMWETA
WANMM

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdori Mpango ameielekeza Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na ile ya Ulinzi kwenda eneo la Oldonyosambu lilipo wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha kusikiliza na kutafuta suluhu ya changamoto ya wananchi na shamba la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdori Mpango akimpa maelekezo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda wakati aliposimama eneo la Oldonyosambu wilayani Arumeru mkoa wa Arusha kusikiliza kero za wananchi tarehe 10 Februari 2024.

Dkt.Mpango ametoa maelekezo hayo tarehe 10 Februari 2024 katika eneo la oldonyosambu aliposimamishwa na wananchi barabarani wakitaka kusikikizwa changamoto zinazowakabili wananchi wa eneo hilo ikiwemo ya maji, barabara, umeme na shamba la Jeshi la Kujenga Taifa.
Sehemu ya wananchi wa eneo la Oldonyosambu wilayani Arumeru mkoa wa Arusha waliojitokeza kumsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdori Mpango tarehe 10 Februari 2024.

Katika kutoa majibu ya mgogoro huo. Dkt Mpango aliwaambia wananchi hao kuwa, anawaelekeza mawaziri wa wizara hizo mbili kwenda eneo husika kwa lengo la kukutana na kuwasikiliza wananchi wa eneo hilo ili kutafuta suluhu ya mgogoro huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdori Mpango akizungumza na wananchi wa eneo la Oldonyosambu wilayani Arumeru mkoa wa Arusha tarehe 10 Februari 2024.

"Naibu Waziri wa Ardhi, nakutaka urudi hapa ukiwa na mwenzako Waziri wa Ulinzi ulimalize jambo hili," alisema Mhe Dkt.Mpango.

Awali wakati wa mkutano wa hadhara mara baada ya Makamu wa Rais Mhe Dkt Mpango kuzindua miradi ya umeme na kituo cha Afya Ketumbeine, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda aliwaeleza wananchi wa Longido kuwa, wilaya hiyo kwa sasa iko shwari kwa kuwa changomoto pekee iliyopo katika eneo la ardhi ni ile ya mipaka ya wilaya aliyoieleza kuwa inafanyiwa kazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdori Mpango akisalimiana na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda alipowasili wilayani Longido kuzindua mradi wa REA na Kituo cha Afya cha Ketumbeine tarehe 10 Februari 2024.

"Migongano hapa Longido imetulia na changamoto iliyopo ni ya mipaka ya wilaya na zipo timu zinafanyia kazi, niwashukuru wakuu wa wilaya kwa kazi kubwa ya kuwapa utulivu wananchi " alisema Mhe Pinda.

Aidha, Mhe. Pinda ameonya wale wote wanaovamia maeneo ya ardhi na kuahidi wizara yake kushirikiana na wakuu wa wilaya katika kudhibiti uvamizi huo huku akitoa wito kwa watanzania kuwa, ardhi haiongezeki pamoja na idadi ya watu kuongezeka na kutaka busara kutumika katika kuitumia ardhi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdori Mpango akipiga makofi na viongozi wengine baada ya kuzindua mradi wa REA wilayani Longido tarehe 10 Februari 2024. Kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).

Katika ziara yake wilayani Longido Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Isdori Mpango alizindua kituo cha afya Ketumbeine, Mradi wa REA pamoja na kuweka jiwe la msingi kwenye shule ya Sekondari Wasichana ya Longido Samia Suluhu Hassan.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news