Ajinasua kwenda jela kisa kutaka kujinufaisha kwa fedha za Kikundi cha Walemavu Liparamba

RUVUMA-Katibu wa Kikundi cha Walemavu Liparamba kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma,Rainely Mathias Ngonyani amenusurika kwenda jela miaka miwili baada ya kulipa faini ya shilingi 100,000.
Ni baada ya Machi 21, 2024 katika Mahakama ya Wilaya Nyasa, mbele ya Mheshimiwa Hakimu Osmund Nsackhatu Ngatunga kuamriwa kesi ya rushwa namba 6013/2024.

Kesi hiyo ilikuwa ni ya Jamhuri dhidi ya Bw. Ngonyani ambaye ni katibu wa kikundi hicho.

Mshitakiwa alishtakiwa kwa kosa la ubadhilifu kinyume na Kifungu cha 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 mapitio ya 2022 ikisomwa pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 mapitio ya 2022.

Katibu huyo alidaiwa kujipatia manufaa shilingi 2,000,000 fedha za Kikundi cha Walemavu Liparamba walizopewa kutoka Akaunti ya Halmashauri ya Wilaya Nyasa kwa ajili ya kina mama, watoto na walemavu.

Hivyo,kufanya upotevu wa kiasi hicho ambacho ni mali ya Halmashauri ya Nyasa.

Kesi iliongozwa na Wakili Mwandamizi Mwinyi Yahaya ambapo mshtakiwa alitiwa hatiani kwa kukiri kosa lake na kuthibitisha kuwa amesharejesha fedha shilingi 2,000,000 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa.

Licha ya kuomba kupata adhabu nafuu kwa kuwa ni kosa lake la awali na ni mlemavu.

Mahakama ilimhukumu mshtakiwa adhabu ya kulipa faini ya shilingi 100,000 au kifungo cha miaka miwili jela. Aidha,mshtakiwa alilipa faini na kuachiwa huru.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news