Aliyeomba rushwa ya shilingi 120,000 afikishwa mahakamani Kinondoni

DAR ES SALAAM-Machi 12, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam imefunguliwa kesi ya Jinai Namba (Cc.6600) dhidi ya Bw.Benjamin Charles Chuma.
Ni kwa mashtaka ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15(1)(a) na 15(2), cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [CAP 329 RE 2019].

Imedaiwa, mshtakiwa akiwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilungule Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, aliomba rushwa kiasi cha shilingi 120,000 na kupokea kiasi cha shilingi 100,000 ili asimchukulie hatua za kisheria, Bw.Yuredi Mteseli Rwebugisa.

Mshtakiwa alisomewa mashtaka yake mbele ya Mheshimiwa Erick Rwehumbiza na alikana makosa yote.

Hata hivyo,shauri hilo limepangwa tena kusikilizwa Machi 28,2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news