Balozi Kasike akutana na ujumbe kutoka ICM, yaonesha utayari kushirikiana na NFRA

MAPUTO-Mheshimiwa Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji amekutana na Ujumbe wa Taasisi ya Nafaka ya Msumbiji (ICM) uliyoongozwa na Mkurugenzi Mkuu, Bw. Alfredo da Piedade João Nampuio, tarehe 29 Februari, 2024.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo jijini Maputo, Msumbiji.
Ujumbe huo ulifika katika Ofisi za Ubalozi kwa ajili ya kujitambulisha na kuwasilisha ombi la kutaka kuanzisha Ushirikiano kati yake na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) nchini Tanzania.
Pamoja na mambo mengine, ushirikiano huo utawezesha upatikanaji wa soko la mahindi nchini Msumbiji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news