Balozi Kasike ateta na Gavana wa Zambezia

MAPUTO-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji,Mheshimiwa Phaustine Kasike amekutana na Gavana wa Jimbo la Zambezia, Mhe. Pio Augusto Matos kwenye Ofisi za Ubalozi zilizopo Jijini Maputo.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 22,2024 na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo,Msumbiji
Wakati wa mkutano huo, viongozi hao wawili walizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji.
Aidha, kupitia mkutano huo, Mhe. Balozi Kasike alimueleza Mhe. Gavana Matos changamoto mbalimbali zinazowakabili Diaspora wa Tanzania waliopo jimboni Zambezia na kumuomba asaidie katika kuzitafutia ufumbuzi.
Mhe. Gavana Matos alipokea ombi hilo na kumuahidi Mhe. Balozi Kasike kwamba uongozi wa jimbo lake utakutana na Watanzania hao hivi karibuni ili kujadiliana namna ya kumaliza changamoto zinazowakabili, lengo ikiwa ni kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kidugu kati ya Tanzania na Msumbiji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news