Balozi Kasike ateta na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Joaquim Chissano

MAPUTO-Katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji katika sekta ya elimu, Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji amekutana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Joaquim Chissano, Prof. José Magode kwenye ofisi za chuo hicho zilizopo jijini Maputo.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 22,2024 na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo,Msumbiji.
Katika mkutano huo, pamoja na masuala mengine ya ushirikiano, Viongozi hao wawili walikubaliana kuanzishwa Darasa la Lugha ya Kiswahili Chuoni hapo ambapo Ubalozi uliahidi kusaidia kupatikana kwa Walimu watakaofundisha darasa hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news