Balozi Kasike ateta na Naibu Waziri Mkuu wa Eswatini

MBABANE-Mheshimiwa Balozi Phaustine Kasike amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Ufalme wa Eswatini, Mhe. Thulisile Dladla.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 30,2024 na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo,Msumbiji.
Mazungumzo hayo yalifanyika Machi 28, 2024 jijini Mbabane ambapo Mhe. Balozi Kasike alikwenda kumsalimia Mhe. Dladla wakati akiendelea na ziara yake ya kikazi nchini Eswatini.
Wakati wa mazungumzo hayo, Mhe. Dladla, aliahidi kwamba Serikali yake itatoa kila aina ya ushirikiano kwa Mhe. Balozi Kasike ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Kwa upande wake, Mhe. Balozi Kasike aliishukuru Serikali ya Ufalme wa Eswatini kwa ushirikiano aliopata wakati wote akiwa nchini Eswatini na kusisitiza umuhimu wa kutekelezwa masuala yote yaliyokubalika wakati wa ziara hiyo kwa maslahi ya Serikali na wananchi wa Tanzania na Eswatini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news