Tanzania, Eswatini zakubaliana

MBABANE-Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ufalme wa Eswatini zimekubaliana kuimarisha Uhusiano wa Kidiplomasia.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 30,2024 na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo,Msumbiji.

Hayo yalielezwa Machi 28,2024 wakati wa Mkutano kati ya Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Msumbiji, Eswatini na Madagascar na Mhe. Pholile Shakantu, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufalme wa Eswatini uliofanyika jijini Mbabane.
Ili kufanikisha azma hiyo, viongozi hao wamekubaliana kuanzisha mchakato wa kusainiwa Mkataba wa kuanzisha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) inayohusisha sekta mbalimbali baina ya nchi hizo mbili.
Mhe. Balozi Kasike yuko Ufalme wa Eswatini kwa ajili ya kukutana na Viongozi wa Serikali na Taasisi mbalimbali kwa ajili ya kujadiliana masuala ya ushirikiano, hususan kwenye sekta ya Uchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news