Balozi Kasike ateta na Rais wa Chemba ya Biashara Msumbiji

MAPUTO-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji,Mheshimiwa Phaustine Kasike ameteta na Rais wa Chemba ya Biashara ya Msumbiji, Bw Alvaro Massinga.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, mazungumzo hayo yamefanyika Machi 19, 2024 kwenye Ofisi za Chemba hiyo zilizopo jijini Maputo ambapo yalijikita katika utekelezaji na uimarishaji wa Diplomasia ya Uchumi..
Aidha, kupitia mkutano wao, viongozi hao wawili walizungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano katika Sekta ya Biashara na Uwekezaji kwa maslahi ya nchi hizi mbili.

Vile vile,kuzingatia uhusiano wa kidugu na wa kihistoria baina ya Tanzania na Msumbiji ambapo viongozi hao walikubaliana juu ya umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uchumi.
Sambamba na kuzishauri taasisi zinazohusika na masuala ya Uchumi, Biashara na Uwekezaji kufanya kazi kwa ukaribu ikiwemo kushiriki katika maonesho na matukio mengine muhimu ya kiuchumi yanayofanyika katika nchi hizo kila mwaka ikiwemo Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba (Tanzania) na Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Maputo-FACIM (Msumbiji).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news