BoT yafanya majadiliano na OR-TAMISEMI kuhusu mwenendo wa sekta ya huduma ndogo za fedha nchini

DAR ES SALAAM-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeendesha kikao kazi cha majadiliano na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kuhusu mwenendo wa sekta ya huduma ndogo za fedha nchini.
Kikao kazi hicho kimefanyika Machi 11,2024 makao makuu ndogo ya BoT jijini Dar es Salaam.

Aidha,kikao hicho kilichoongozwa na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Sekta za Fedha, Bw. Sadati Musa, kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Ustawi wa Huduma Jumuishi ya Fedha, Bw. Kennedy Komba, kilihusisha pia watendaji kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa ngazi ya Mkoa wa Dar es Salaam na halmashauri za Kigamboni na Ilala.
Kikao hicho kililenga kujenga uelewa wa namna Benki Kuu inavyosimamia sekta ya huduma ndogo za fedha pamoja na majukumu ya OR-TAMISEMI katika masuala ya kusimamia na kuratibu sekta hiyo.
Pia, wadau hao walijadili changamoto mbalimbali zinazowakabili katika usimamizi na uratibu wa sekta hiyo pamoja na kupendekeza namna ya kutatua changamoto hizo ili kuongeza usalama, uimara pamoja na ustawi wa huduma jumuishi za fedha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news