Burundi yaonesha shauku kubwa reli ya SGR kutoka Tanzania

JOSEPH MAHUMI NA JOSEPHINE MAJURA

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Miundombinu wa Burundi, Mhe. Dieudonné Dukundane, kuhusu maendeleo ya Mradi wa Reli ya Kisasa SGR utakaoziunganisha nchi hizo mbili.
Ujumbe wa Tanzania (Kushoto) ukiongozwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati kushoto), na Ujumbe wa Burundi ukiongozwa na Waziri wa Miundombinu na Makazi, Mhe. Dieudonne Dukundane (katikati kulia), wakiwa katika kikao cha pamoja, kilichofanyika jijini Dodoma, kilichojadili kuhusu Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) itakayounganisha nchi hizo mbili. Waliohudhuria kutoka ujumbe wa Tanzania walikuwa Kamishna wa Usimamizi wa Madeni Bw. Japhet Justine (wa kwanza), Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Bw. Robert Mtengule, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Bw. James Msina na Mchumi kutoka Idara ya Fedha za Nje, Bw. Frank Mangap, na kwa upande wa Burundi, ni Balozi wa Burundi nchini Tanzania Mhe. Leontine Nzeyimana (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Mipango na Usanifu Eng. Pasteur Bisekere.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Dodoma, Viongozi hao wamesema kuwa mradi huo utakapokamilika utachochea biashara ya madini na kilimo pamoja na kuimarisha mahusiano ya kikanda na kukuza uchumi wa nchi hizo mbili

Dkt. Nchemba alisema kuwa Ushirikiano wa nchi hizo mbili katika maandalizi ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) umekua mzuri na kwamba watalaamu wa pande zote mbili wameendelea na vikao hususan katika eneo la manunuzi na fedha ili kuhakikisha kila kitu kinafanikiwa.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati wa kikao na Ujumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi ikiongozwa na Waziri wa Miundimbinu na Makazi, Mhe. Dieudonne Dukundane (hayupo pichani), ambapo wamejadiliana kuhusu ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) itakayounganisha nchi hizo mbili ambayo itachochea shughuli za kiuchumi. Kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma, kimehudhuriwa pia na Balozi wa Burundi nchini, Mhe. Leontine Nzeyimana, Mkurugenzi wa Mipango na Usanifu kutoka Wizara ya Miuondombinu na Makazi Burundi, Mhandisi Pasteur Bisekere, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni Bw. Japhet Justine (wa kwanza), Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Robert Mtengule, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. James Msina na Mchumi kutoka Idara ya Fedha za Nje, Bw. Frank Mangap.
Waziri wa Miundimbinu na Makazi Mhe. Dieudonne Dukundane, akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (hayupo pichani) kilichofanyika jijini Dodoma, ambapo alieleza kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo shughuli za kiuchumi na miundombinu.

“Ujenzi wa Reli hii ya Kisasa ya kuunganisha nchi zetu ni muhimu sana kwetu na maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa ni mradi wa kipaumbele na anataka ukamilike,"aliongeza Mhe Dkt. Nchemba.

Alisema kuwa wataalum kutoka nchi hizo mbili wanaendelea kushirikiana ili kuhakikisha kila kitu kinafanikiwa na kufikia matarajio ya Rais wa Tanzania pamoja na Rais wa Burundi ya kuona mradi huo unafanikiwa.

Naye Waziri wa Miundombinu na Makazi wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Dieudonné Dukundane, alisema kuwa nchi yake itahakikisha kuwa mradi huo unapewa kipaumbele na tayari timu ya wataalam kutoka Burundi ipo Dar es Salaam ikiendelea kupitia masuala ya manunuzi wakishirikiana na wataalam wa Tanzania.

“Rais wangu Mhe. Evariste Ndayishimiye, ametuelekeza kuwa tufuatilie kwa ukaribu na kwa kipaumbele mchakato mzima unakwenda kama ilivyopangwa ili uishe vizuri, na mimi nimeishi hapa Tanzania kwa miaka sita (6) nimeona namna ambavyo SGR itakavyoharakisha maendeleo ya nchi,” alisema Mhe. Dukundane.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Miundombinu na Makazi Mhe. Dieudonne Dukundane baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika jijini Dodoma, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) itakayounganisha nchi hizo mbili ambayo itachochea shughuli za kiuchumi.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (kushoto) akiagana na Waziri wa Miundimbinu na Makazi Mhe. Dieudonne Dukundane baada ya kumalizika kwa kikao, kilichofanyika jijini Dodoma, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano ukiwemo Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) itakayounganisha nchi hizo mbili ambayo itachochea shughuli za kiuchumi.
Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wapili kushoto), Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni, Bw. Japhet Justine (wa kwanza) Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Robert Mtengule, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Bw. James Msina na Mchumi kutoka Idara ya Fedha za Nje Bw. Frank Mangapi wakiwa katika kikao kilichomshirikisha Waziri wa Miundombinu na Makazi kutoka Burundi Mhe. Dieudonne Dukundane (hayupo picha), kilichofanyika jijini Dodoma.

Mradi huo wa Reli ya Kisasa (SGR) baada ya kukamilika hususan Ujenzi wa Reli ya Uvinza hadi Musongati nchini Burundi kutawezesha kusafirisha tani milioni 3 za madini kwa mwaka kutoka mgodi mkubwa wa madini ya Nickel uliopo Musongati nchini Burundi unaokadiriwa kuwa na hifadhi ya tani milioni 150 za madini ya Nickel, Cobalt na Copper, na pia kuimarisha shughuli za kiuchumi za nchi hizo mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news