BREAKING NEWS:Rais Dkt.Samia ateua, atengua vigogo usiku huu

NA GODFREY NNKO 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Ally Senga Gugu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani. Kabla ya uteuzi huo, Gugu alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Machi 15,2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus.

Aidha, amemteua Kaspar Kaspar Mmuya kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma. Kabla ya uteuzi huo,Mmuya alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani.

Wakati huo huo, Rais Dkt.Samia amemteua Mhandisi Mwajuma Waziri kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji. Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Waziri alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji.

Mhandisi Waziri anachukua nafasi ya Profesa Jamal Katundu ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Pia, amemteua Ephraim Mafuru kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Mafuru anachukua nafasi ya Damasi Mfugale ambaye uteuzi wake umetenguliwa, kabla ya uteuzi huu Mafuru alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia ametengua uteuzi wa Richard Rwanyakaato Kiiza, Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA).




Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news