DCEA yafikisha elimu kuhusu dawa za kulevya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA)

ARUSHA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha pamoja na wadau wengine wamefanya kongamano la vijana katika kupinga rushwa na dawa za kulevya katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kilichopo Njiro jijini Arusha.
Mgeni rasmi wa Kongamano hilo alikuwa Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha, Bi. Zawadi Ngailo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongella.
Jumla ya washiriki 547 walihudhuria kongamano hilo; ikihusisha wanafunzi wa shule tisa za Sekondari kutoka Wilaya ya Arumeru na Jiji la Arusha, waraibu wanawake, na wadau wengine mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news