Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Machi 12,2024

DODOMA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, kwenye Kamati ya Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, ambapo Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 49.34 kwa mwaka 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/24 ya shilingi trilioni 44.39.

Hafla hiyo imeongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na kuhudhuriwa pia na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Doto Biteko na Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azan Zungu.










Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news