Kamati yapitisha makadirio ya bajeti Ofisi ya Waziri Mkuu mwaka 2024/25

DODOMA-Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akiwasilisha Taarifa kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2024/25, kikao kilifanyika bungeni jijini Dodoma mbele ya kamati ya kudumu ya utawala na Katiba na Sheria.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Florent Laurent Kyombo akikaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo hiyo Machi 19, 2024 katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma.

Ni baada ya wajumbe kujadili na kuridhia bajeti katika kikao kilichohusisha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Wakuu wa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo, wataalamu kutoka Idara na Vitengo vya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Alieleza kuwa, bajeti ya ofisi hiyo iwe yenye matokeo chanya na kusaidia kuleta maendeleo kwa wananchi huku akiipongeza Ooisi kwa kazi kubwa ya uratibu wa shughuli za Serikali.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Katiba na Sheria Mhe. Florent Laurent Kyombo (akikaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo) akiongoza kikao cha kamati hiyo katika Ukumbi wa Bunge kuhusu kupokea Taarifa kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2024/25, kilichofanyika tarehe 19 Machi, 2024.Kulia kwake ni Katibu wa kamati hiyo Bw. Frank Nkya.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza jambo wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2024/25.

“Kipekee kamati imepitisha makadirio ya bajeti hii muhimu mara baada ya kusikia wasilisho na kujadili kwa kina, tunashukuru kwa wasilisho endeleeni na jukumu la uratibu wa shughuli za Serikali kwa manufaa ya jamii katika kujiletea maendeleo,” alisema Makamu Mwenyekiti huyo.

Awali akiwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/25 mbele ya kamati hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama ameishukuru kamati kwa kujadili na kupitisha makadiri ya bajeti hiyo huku akisema Ofisi yake itaendelea kufanya kazi kwa weledi zaidi kwa kuzingatia jukumu la msingi la Uratibu wa Shughuli zote za Serikali.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza jambo wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Ramadhan Kailima akizungumza jambo wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Katibu Tawala wa Njombe Bi. Judica Omari wakati alipowasili kushiriki kikao cha wa kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria katika Ukumbi wa Bunge kilichofanyika tarehe 19 Machi, 2024.

Pia Waziri Mhagama alisema mpango wa shughuli zitakazotekelezwa kwa kutumia bajeti hiyo ya mwaka wa fedha ujao 2024/25 ambapo wanakamati kwa kauli moja walipitisha makadirio ya bajeti hiyo.

“Ni imani yangu kuwa bajeti hii itakapopita tunakwenda kutekeleza malengo yetu huku tukihakikisha shughuli mbalimbali ikiwemo za uratibu wa masuala ya maafa, uratibu wa shughuli za bunge, masuala ya tathmin na ufuatiliaji wa shughuli za Serikali pamoja jukumu la uendelezaji wa Mji wa Serikali Mtumba Dodoma unaendelea vizuri ikiwa ni moja ya majukumu katika kuratibu,”alisema Mhe.Mhagama.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Katiba na Sheria Mhe. Abeid Ighondo Ramadhan akichangia jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Mashimba Ndaki akichangia jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo.

Akizungumza kuhusu masuala ya Ofisi ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali alihakikishia Kamati kuwa wataendelea kuboresha mitambo na kuisimamia vyema ili kuhakikisha kila nyaraka za Serikali ziendelee kuchapwa kwa Mpigachapa Mkuu wa Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news