Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati afanya kikao na wawakilishi kutoka Energy Cards

DAR ES SALAAM-Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amekutana na Wataalam kutoka Taasisi ya Energy CARDS ambao walifika ofisini kwake kwa ajili ya kutambulisha shughuli wanazozifanya.
Katika kikao kilichofanyika tarehe 7 Machi, 2024 jijini Dar es Salaam, Wataalam hao walieleza kuwa Taasisi hiyo inajishughulisha na masuala ya kutoa ushauri wa kitaalam (consultancy) hususani kwenye masuala ya Nishati katika gesi, petroli na nishati jadidifu.

Katibu Mkuu aliwapongeza Wataalam hao na kuwahakikishia kuwa Wizara iko tayari kuwatumia wataalam wa ndani kwa ajili ya miradi mbalimbali.

Baadhi ya Wataalam kutoka Taasisi hiyo ni Gabriel Bujulu, Edward Ishengoma, Mary Pancras, Adam Zuberi, Helen Lyimo, Mha. Kato Kabaka na Jacob Mayalla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news