Mufti awaalika waumini kumuombea hayati Ali Hassan Mwinyi

DAR ES SALAAM-Mufti wa Tanzania,Dkt. Abubakar Zubeir Ali Mbwana amewaalika waislamu na waumini wote kuhudhuria dua kumuombea Rais wa Awamu ya pili Almargoum Ali Hassan Mwinyi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu Mkuu wa BAKWATA, Alhaj Nuhu Jabir Mruma dua hiyo itafanyika kesho saa saba mchana kwenye Msikiti wa mfalme Mohammed VI Bakwata Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Alhaj Mruma amewataka viongozi wa taasisi na madhehebu mbalimbali na viongozi wa BAKWATA mikoa na wilaya kudhuria na hasa viongozi wote wa BAKWATA Dar es Salaam wa Ngazi ya mkoa, wilaya zote, kata na maimamu wa jiji la Dar es salaam pamoja na waumini wote.

Alhaj Mruma amesema,maandalizi yote yamekamilika na kwamba waumini wote ni vyema wafike mapema ili kujumuika pamoja kuanzia mwanzo wa Dua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news