Musoma Vijijini wapanda miti shuleni

NA FRESHA KINASA

LEO Machi 21,2024 ni siku ya Umoja wa Mataifa (UN) ya kukumbushana umuhimu wa misitu ya aina zote.
UN ilipitisha azimio la siku hii ya tarehe 21 Machi ya kila mwaka) kwenye Mkutano wake wa tarehe 28 Novemba,2013. Ambapo kauli mbiu 2024 inasema 'Misitu na Ubunifu'

Katika kutekeleza kauli mbiu hii kwa vitendo Jimbo la Musoma Vijijini,kwa muda wa zaidi ya wiki mbili kupitia Mbunge wa Jimbo hilo,Prof. Sospeter Muhongo akishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Halfan Haule, na Meneja wa Misitu (TFS) Wilaya, Ndugu Boniphace Kaberege wamekuwa wakigawa na kupanda mamia ya miche ya miti.
Miti hiyo ni ya matunda, mbao na kivuli kwenye shule kadhaa za misingi na sekondari za jimboni humo ambapo kampeni hii ni endelevu jimboni humo.

Ambapo sherehe ya uzinduzi wa upandaji miti ilifanyika tarehe 20 Machi,2024.

TFS wilaya chini ya uongozi wa Ndugu Boniphace Kaberege ilitoa mafunzo ya umuhimu wa misitu kwa maisha na ustawi wa jamii zetu.
Mafunzo hayo yalifanywa kwenye Sekondari ya Suguti Wilaya ya Musoma.

Wanafunzi na walimu wote wa sekondari hiyo, wakiongozwa na Mkuu wao, Mwalimu Pendo Kaponoke walihudhuria mafunzo hayo. Huku wakipongeza jitihada zinazofanywa na Mbunge Prof. Muhongo katika utunzaji wa mazingira.

Aidha, Wanavijiji wa Kata ya Suguti (Vijiji 4 vya Chirorwe, Kusenyi, Suguti na Wanyere) walihudhuria, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Alphonce Wambura.
Wanufunzi 100 wa Sekondari hii ya Suguti wamekuwa, Mabalozi wa Mazingira (Environmental Ambassadors) chini ya Mwalimu wao wa Mazingira, Mwl Keneth Elias. Hawa wataongoza Kampeni ya upandaji na utunzaji miti ndani ya Kata ya Suguti, na kwingineko Jimboni humo.

Aidha, uzinduzi wa Upandaji na Utunzaji miti kwenye shule zote Jimboni humo umefanywa tarehe 20.3. 2024 na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Meneja wa TFS Wilaya walizindua kampeni endelevu ya upandaji na utunzaji wa miti kwenye shule zote za Jimboni humo. Na uzinduzi huo ulifanyika Suguti Sekondari.

Paulo Fabiani Mkazi wa Suguti amesema kwamba, ni muda mwafaka Sasa kwa Wananchi jimboni humo kushikamana na Mbunge wao na Serikali katika agenda ya utunzaji mazingira kwa kupanda miti katika maeneo yao na taasisi za umma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news