Mwalimu Mkuu hatiani Kagera kwa kuomba hongo amuombee raia wa Uganda cheti cha kuzaliwa na namba ya NIDA

KAGERA-Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba mkoani Kagera imemhukumu,Mwalimu wa Shule ya Msingi Kahaazi na mmiliki wa Mpendekelaki Stationary, Bw.Naswiru Mpendekelaki kwa kuomba hongo ili amuombee raia wa Uganda cheti cha kuzaliwa na Namba ya NIDA.
Mshitakiwa ametiwa hatiani na kuamriwa alipe faini ya shilingi 500,000 au kwenda jela miaka miwili kwa kuomba na kupokea hongo ya shilingi 300,000.

Ilidaiwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na Kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329.

Hukumu hiyo dhidi ya Naswiru Mpendekelaki katika kesi ya Rushwa namba 7824/2024 imetolewa Machi 22,2024 chini ya Mhe. Andrew Kabuka, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bukoba.

Ilidaiwa kwamba mshtakiwa akiwa mwalimu wa Shule ya Msingi Kahaazi na mmiliki wa Mpendekelaki Stationary, aliomba na kupokea rushwa ya shilingi 300,000 kutoka kwa John Bosco Balija ambaye ni raia wa Uganda ili aweze kumuombea cheti cha kuzaliwa na namba ya NIDA katika mamlaka husika.

Aidha,mshitakiwa amelipa faini na kuachiwa huru na Mahakama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news