Mwenyekiti wa Kijiji aichokoza Serikali kwa kuomba hongo ya shilingi 60,000

MANYARA-Mwenyekiti wa Kijiji cha Nasetan, Kata ya Engusero Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara, Mambe Mohamed Mambe ameichokoza Serikali kwa kuomba hongo.
Mshtakiwa ametiwa hatiani na kuamriwa kwenda jela miaka minne au kulipa faini ya shilingi 1,000,000 kwa makosa ya kuomba na kupokea hongo kiasi cha shilingi 60,000.

Kitendo hicho ni kinyume na Kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Hukumu hiyo dhidi ya Mambe katika kesi ya jinai Na.20/2023, imetolewa Machi 27,2024 na Mhe. Boniface Lihamwike, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kiteto.

Mshtakiwa aliomba hongo ya sh. 60,000 ili asimchukulie hatua za kisheria mwananchi ambaye alifanya mkutano wa wafugaji bila kibali cha serikali ya kijiji.

Mshtakiwa ameshindwa kulipa faini na amepelekwa magereza kutumikia kifungo chake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news