Rais Dkt.Mwinyi abainisha aliyojifunza kwa baba yake wakati wa uhai wake

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametaja baadhi ya mambo aliyojifunza kutoka kwa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,hayati Ali Hassan Mwinyi wakati wa uhai wake.
"Hayati mzee Mwinyi alikuwa na subira kubwa wakati alipokuwa kiongozi hususani kipindi cha mageuzi ya kisiasa na kiuchumi.

Pia,watu walimsema vibaya kwa mambo ya kutunga katika vyombo vya habari,lakini hakuwahi kumjibu yeyote kwa mabaya waliyomsema."

Alhaj Dkt.Mwinyi ameongeza na kusema yeye amejifunza kusubiri kwa fundisho alilolipata kwa mzee wake kwa kumpa mafunzo mema.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema wakati marehemu baba yake alipokuwa akitibiwa Uingereza aliwataka madaktari na familia arudishwe nyumbani na baadae apelekwe Zanzibar, maneno hayo aliyarudiarudia hata baada ya kufika Dar es Salaam.

RaisDk.t. Mwinyi ameyasema hayo katika dua ya hitma iliyoandaliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,hayati Ali Hassan Mwinyi ambayo imefanyika leo Machi 5,2024, Msikiti wa Zinjibar Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Rais Dkt.Mwinyi ameishukuru Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Mazishi inayoongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar,Mhe. Hemed Suleiman Abdulla pamoja na wajumbe wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news