Rais Dkt.Mwinyi atoa rai kwa vikosi vya ulinzi na uslama

ZANZIBAR-Kamanda Mkuu wa Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Maafisa, Askari na Wapiganaji wa Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kudumisha nidhamu, uzalendo, uwajibikaji na uadilifu.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Machi 10,2024 akizungumza na Maafisa, Askari na Wapiganaji alipotembelea Kikosi cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) Kibweni na Kikosi cha KVZ Mtoni Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Vikosi vya SMZ na kuhitimisha.
Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM) na Kikosi cha KVZ kwa utekelezaji wa kazi nzuri za ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayofanywa na Serikali.
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ya vikosi hivyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news