Rais Dkt.Mwinyi azindua fursa za uchimbaji mafuta na gesi Zanzibar

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali inapenda kuzialika kampuni zote za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi kushiriki katika duru ya kwanza.
Pia,Rais Dkt.Mwinyi amewahakikishia wawekezaji wote wa sekta ya mafuta na gesi kuwa, Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwa manufaa ya wote.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Machi 20,2024 katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip iliyopo Uwanja wa Ndege alipozindua duru ya kwanza ya utoaji wa vitalu kwa kampuni za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia maeneo ya baharini Zanzibar.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa, dhamira ya Serikali katika uchumi wa buluu ni kuimarisha uchumi wa nchi kwa haraka na kuhakikisha upatikanaji wa maendeleo endelevu ya vyanzo vya nishati ya uhakika.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesema, Serikali inaamini kuwa uchumi wa Buluu una fursa nyingi za kukuza mipango ya maendeleo ya kiuchumi yenye lengo la kupunguza umasikini na kutengeneza fursa za ajira nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news