Simba SC yasema imechoka kuishia robo fainali

DAR ES SALAAM-Msemaji wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam,Ahmed Ally amesema, wamechoka kuishia robo fainali michuano ya Kimataifa.

Ameyasema hayo leo Machi 27,2024 Mbagala jijini Dar es Salaam kwenye muendelezo wa hamasa ya kuelekea kwenye mchezo wa robo fainali Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Ahly siku ya Ijumaa.

“Hili ni jambo letu sisi, hii ni mechi yetu sisi na sisi lengo letu ni moja tu kushinda. Tunachotaka ni kwenda nusu fainali, sio kingine chochote.

"Sisi tunasema pamoja na ubora, ukubwa, mafanikio waliyonayo lakini tarehe 29 tunakwenda kupambana nao. Safari hii tumedhamiria, tumeshachoka kuishia robo.
“Kwa ubora tulio nao, kwa wachezaji tulionao, kwa makocha tulionao wakiongozwa na Benchikha tunaitaka nusu fainali. Tunataka kuimaliza kazi hii Uwanja wa Mkapa ili tukienda Misri kazi inakuwa nyepesi.

“Wanasimba wote tunawahitaji tarehe 20 kwenye dimba la Mkapa, twende tuunganishe nguvu tuipeleke Simba nusu fainali. Mechi hii inawahitaji Wanasimba wote kwa pamoja. Safari hii tunaitaka nusu fainali.

“Mwaka huu tumedhamiria vyovyote iwavyo lazima twende nusu fainali. Cha kufanya sisi Wanasimba ni kununua tiketi zetu Ijumaa kwa Mkapa panatuhusu.

"Na Ijumaa ni sikukuu, hakuna kazi. Watu wote tunakwenda uwanjani na tunachokitaka ni kuimaliza mechi hii hapa Tanzania.

“Kikosi chetu kipo kwenye hali nzuri sana, tulipata wiki moja ya kujiandaa tukiwa Zanzibar na sasa tuna mazoezi ya leo na kesho kumalizia maandalizi. Mpinzani wetu amefika leo mchana. Tarehe 29 atacheza mechi ngumu ambayo hajawahi kukutana nayo.

“Uwezo wa kuwatoa tunao lakini uwezo huo utachagizwa na Wanasimba kwenda uwanjani. Mkiamua tunamtoa mapema. Niwakumbushe tena hii sio mechi ya bure, hii ni mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kila mtu ataingia kwa kiingilio chake,"amesema Ahmed Ally.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news