Kamati ya Bunge yakagua ujenzi wa ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali jijini Dodoma


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ikikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwenye Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.
Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Mark Mulwambo akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na wajumbe wake wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Mary Makondo akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kabla ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Florent Kyombo.
Mhandisi wa mradi wa SUMA JKT, Mhandisi Baraka Mosha akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Yahaya Masare akisisitiza jambo kwa Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Mark Mulwambo (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.
Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Mark Mulwambo akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kabla Kamati hiyo kuanza kukagua ujenzi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali unaoendelea kufanyika kwenye Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ujenzi ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakifuatilia kikao baina yao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa Ofisi hiyo kwenye Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.
Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Mark Mulwambo akifafanua jambo kwa Mhe. Abdallah Mwinyi, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua ujenzi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.
Kaimu Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Mark Mulwambo (kushoto) akifafanua jambo kwa Mhe. Abdallah Mwinyi, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua ujenzi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.
Picha ya pamoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria; viongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria; watendaji wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali; mkandarasi SUMA JKT; na mshauri elekezi TBA baada ya kukagua ujenzi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news