TEF yaomboleza kifo cha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi

DAR ES SALAAM-Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeelezea kumepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Rais mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia Februari 29, 2024.

Ni katika Hospitali ya Mzena, Kijitonyama jijini Dar es Salaam alikokuwa anapatiwa matibabu.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa TEF,Deodatus Balile leo Machi 1,2024.

"Mzee Mwinyi katika uongozi wake alianzisha demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa Tanzania, aliondoa vikwazo kwa kampuni binafsi, akapunguza vikwazo vya uagizaji bidhaa kutoka nje, na kupata jina la utani la "Mzee Ruksa",

"Msemo wa Kiswahili ambao unaweza kutafsiriwa kama "Ruhusa ya Mheshimiwa kutenda lililo jema." Aliwafanya Watanzania wajue na kushika fedha katika uongozi wake.

"Alisisitiza uwajibikaji kazini na kukemea wazembe, kwa kuasisi maneno “fagio la chuma” maana wazembe wote walikuwa wakiondolewa kazini au kupunguzwa kazi.

"Ndiye aliyeruhusu watumishi kujitafutia kipato cha ziada baada ya saa za kazi,madaktari wakaanza kufanya kazi kwenye vituo vingine na hata kufungua hospitali zao binafsi.

"Aliamini katika ukuaji wa uchumi kwa mtu mmoja mmoja kwa maendeleo ya familia na taifa.

"Mzee Mwinyi wakati wa uhai wake alichagiza michezo na yeye alikuwa mpenda michezo hasa jogging (kukimbia). Pia alikuwa mwandishi wa mashairi na vitabu.

"TEF tunaungana na familia ya Mzee Ali Hassan Mwinyi na Watanzania wote kuomboleza msiba huu mkubwa kwa taifa.Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya Mzee Mwinyi,"amesisitiza Mwenyekiti wa TEF,Deodatus Balile leo Machi 1,2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news