Wananchi wajenga Kituo cha Polisi Kata ya Mbokomu

KILIMANJARO-Wadau wa maendeleo na masuala ya ulinzi (New Maendeleo Group) wamefanikisha ujenzi wa Kituo cha Polisi katika Kata ya Mbokomu Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro ili kuimarisha ulinzi na usalama wa eneo la kata hiyo huku kamanda wa mkoa huo akiwapongeza kwa kufanya uamuzi sahihi.
Akifungua kituo hicho kilichojengwa kwa nguvu za wananchi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Simon Maigwa amewashukuru wananchi wa Kata ya Mbokomu ambao wamejenga kituo hicho chenye thamani ya shilini milioni thelathini na tano.

SACP Maigwa ameongeza kuwa, kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda raia na mali zao huku akibanisha kuwa wao Jeshi la Polisi wanao wajibu wa kuwalinda wananchi muda wote ambapo ameahidi kuwa ataongeza askari ambao watahudumu katika kituo hicho ili kiwe na matokeo chanya ya kudhibiti uhalifu kama ilivyo kusudi la wananchi waliojenga kituo hicho.
Aidha, Kamanda Maigwa amewakikishia wananchi hao kuwa atahakikisha kuwa wanakuwa salama ambapo amewaomba kutembea kifua mbele huku akisema kuwa mkoa huo ni salama na utaendelea kuwa salama na amewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili mkoa huo uendelee kuwa shwari.

Nao baadhi ya wananchi walioshiriki kujenga kituo hicho wamesema wanaimani kubwa na Jeshi la Polisi huku wakiliomba jeshi hilo kutenda haki kwa wananchi na kutobambikiza kesi wananchi ambao wanalitegemea sana jeshi hilo.
Afisa mnadhimu namba moja Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Abel Mtagwa amesema,jeshi hilo linategemea sana wananchi huku akiwaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za wahalifu ili Jeshi hilo liwafikishe katika vyombo vya sheria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news