TUGHE yaiomba Serikali kuwaongezea siku ya likizo ya uzazi wafanyakazi wanawake wanaojifungua watoto njiti

PWANI-Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) kimeiomba Serikali kufanya mabadiliko katika sheria zake ili kuwaongezea muda wa Siku za Likizo ya Uzazi Wafanyakazi Wanawake wanaojifungua watoto njiti.
Ni ili kutoa fursa ya kuwahudumia watoto hao sambamba na kupata muda wa kupumzika ili wanaporejea kazini waweze kulete tija katika maeneo yao ya kazi.

Wito huo umetolewa na Afisa Elimu Kazi wa TUGHE, Cde. Nsubisi Mwasandende alipoambatana na ujumbe wa wawakilishi kutoka Kamati ya Wawake TUGHE Makao Makuu.
Sambamba na uongozi wa TUGHE Mkoa wa Pwani walipotembelea na kutoa msaada katika wodi ya wanawake waliojifungua watoto njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi tarehe 5 Machi, 2024.

Cde. Mwasandende ameeleza kuwa, sheria ya sasa ya ajira na mahusiano kazini imekuwa ikitoa siku 84 kwa wanawake wanaojifungua mtoto mmoja.
Ikiwemo pia siku 100 kwa wanaojifungua zaidi ya mtoto mmoja na wala haisemi chochote kuhusiana na wanawake wanaojifungua watoto njiti.

Amesema,ndio maana TUGHE imeona ni vyema mara kwa mara kuendelea kuikumbusha Serikali kufanya mabadiliko ambayo wataongeza kipengele kuhusiana na kuongezewa Siku za Likizo ya Uzazi kwa
wanawake wanaojifungua watoto njiti.
“Wapo wanawake wengi watumishi wamekuwa wakijifungua watoto njiti na muda wanaopata kukaa na watoto unakuwa hautoshi.

"Kwa kuzingatia watoto hao huitaji sana uangalizi wa karibu kutoka kwa mama zao ili waweze kukua na pia afya zao kuimarika.

"Hivyo tunaomba sana serikali iweze kuliangalia upya jambo hili kwa kufanya mabadiliko katika sheria zake, alieleza Cde.
Mwasendende.

Kwa upande wa Sekta Binafsi, Cde. Mwasandende amewaomba waajiri nchini katika mikataba yao ya hali bora kuingiza kipingele hiki cha kuongeza muda kwa siku za likizo ya uzazi kwa wanaojifungua watoto njiti.

Ni kama ambavyo mwishoni mwa mwaka jana 2023 Chama cha TUGHE waliweka kipengele hicho katika Mkataba wake wa Hali Bora na kuwa Chama cha kwanza cha Wafanyakazi Nchini kufanya hivyo katika Mkataba wake wa hali bora.
Naye Mwenyekiti wa Wanawake TUGHE Makao Makuu, Cde. Agness Ngereza amesema katika
kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani wameona ni vyema kuwatembelea na kutoa msaada katika wodi ya wanawake wanaojifungua watoto njiti.

Ssambamba na kuzungumza nao kufahamu changamoto mbalimbali zinazowakabili na kutoa wito kwa wadau wengine kufanya matendo ambayo yataigusa jamii yenye uhitaji. Pia ameushukuru uongozi wa hospitali ya Tumbi kwa kuwakaribisha sambamba na kuwapongeza kwa huduma nzuri wanayotoa hospitalini hapo.

Akizungumza kwa niaba ya wanawake waliolazwa wodini hapo ambao wamejifungua watoto njiti,

Dada Sikitu ameushukuru uongozi wa TUGHE kwa kuwatembelea na kuwapa msaada na kuwaomba waendelee kuwasemea changamoto zao pasipo kuchoka mpaka pale zitakapopatiwa
ufumbuzi.

Kwa upande wa Uongozi wa Hospitali hiyo umeipongeza TUGHE kwa kuwakumbuka watoto hao ambao wanahitaji msaada na kutoa rai kwa Watanzania wote kujitoa kwa hali na mali ili kuwawezesha watoto hao kukua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news