Vifaa vya ujenzi Musoma Vijijini kuanza kutolewa kesho

NA FRESHA KINASA

VIFAA vya ujenzi vilivyonunuliwa na fedha za Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini chini ya Mbunge Prof. Sospeter Muhongo vinaanza kugawiwa kesho Machi 12, 2024.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Machi 11,2024 na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

"Fedha ni shilingi milioni 75,769,000. Ambapo vifaa vilivyonunuliwa ni saruji, Twiga Plus Mifuko 2,010, Nondo, 12mm: 311, na Mabati ya rangi: 344, " imeeleza taarifa hiyo na kusema kuwa,

"Kipaumbele cha matumizi ya vifaa hivi ni Ukamilishaj wa ujenzi wa Maabara 3 (Physics, Chemistry & Biology) kwa kila Sekondari ya Kata ndani ya Jimbo letu.

"Sekondari zilizotuma maombi ya saruji na kilichopatikana. Ambapo Makojo imepata mifuko ya saruji 150, Nyasaungu 50 (mpya), Rukuba Kisiwa 205 (mpya), Kigera 100, Nyanja 100, Bulinga 100, Bukwaya 150, Muhoji 50 (mpya),

"Rusoli 100, Busambara 150, Nyambono 150, Mtiro 150, Suguti 100, Etaro 100, Seka 150 na David Massamba Memorial 205 (mpya)," imeeleza sehemu na kuongeza kuwa.

"Uchache wa mabati yaliyonunuliwa, uchache wa mabati ya rangi yaliyonunuliwa, umelazimisha mgao uende kwenye sekondari zenye maboma ya kukamilisha ujenzi wa maabara zao, ambazo ni Etaro (mabati 120), Mabuimerafuru (105) na Mtiro (139).

"Usafirishaji wa vifaa vitakavyogawiwa , Kila Sekondari itajitegemea kusafirisha vifaa vya ujenzi walivyogawiwa kutoka kwenye Bohari ya Halmashauri yetu iliyoko Musoma Mjini,"imeeleza taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news