Walimu wawili Geita mbaroni kwa tuhuma za ubadhirifu

GEITA-Ambakisye Amani Mfwango ambaye ni Mwalimu Mkuu na Beatrice David Musiba ambaye ni mwalimu wa kawaida wote wa Shule ya Msingi Bukandwe wamefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kwa mashtaka ya ubadhirifu wa mali za umma na kugushi nyaraka za vikao.
Machi 18, 2024 wawili hao walifunguliwa shauri la rushwa na uhujumu uchumi Na.7060/2024 mbele ya mheshimiwa hakimu Atupye Benson Fungo ambaye ni Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbogwe.

Walimu hao walifikishwa mahakamani na Ofisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Mbogwe, ikiongozwa na Wakili wa Jamhuri Chali Kadeghe.

Aidha, washitakiwa wamefikishwa mahakamani kwa mashtaka ya ubadhirifu wa mali za umma, kugushi nyaraka za vikao vya Kamati ya Shule ya Msingi Kanegere.

Sambamba na kugushi hati ya malipo yenye thamani ya shilingi 1,500,000 kwa manufaa yao binafsi, jambo ambalo ni kinyume na vifungu vya 333, 335(d)&(i) na 337 vyote vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 iliyorejewa Mwaka 2022.

Makosa hayo pia ni kinyume na Vifungu vya 28(1) na 31 vyote vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11/2011, ikisomwa pamoja na Aya ya 21 ya Jedwali la kwanza, vifungu vya 57(1) na 60(2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 toleo la Mwaka 2022.

Washitakiwa wote walikana kutenda makosa hayo na shauri liliahirishwa hadi Machi 28, mwaka huu litakapo kuja mahakamani hapo kwa ajili ya upande wa Jamhuri kusoma hoja za awali.

Hata hivyo, washitakiwa walishindwa kutimiza mashariti ya dhamana na hivyo kubaki ndani ya mahabusu mpaka watakapotimiza mashariti hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news