Wamasai watoa mkono wa pole kwa Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole Ikulu Migombani kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wamasai waishio Zanzibar (ERETO), Ndg. Thomas Makau Lepachu na ujumbe wake.
Ni kufuatia kifo cha Baba yake Mzazi, Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia Februari 29,2024 wakati akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam na kuzikwa Machi 2,2024 huko Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Jumuiya hiyo wamemkabidhi Mbuzi na Kondoo ikiwa ni sehemu ya rambirambi yao kwa utamaduni wao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news