Watumishi wahukumiwa kwa kuomba hongo ya shilingi 75,000 Mbeya

MBEYA-Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imewahukumu,Bw. Nelson Mwakilasa ambaye ni msaidizi wa Mkuu wa Masoko na Felister Mwanisongole ambaye ni Askari Mgambo, wote hao wakiwa ni watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Watumishi hao wameamuriwa kulipa faini ya shilingi 600,000 kila mmoja au kwenda jela miaka mitatu kwa makosa ya kuomba na kupokea hongo ya shilingi 75,000.

Hukumu dhidi ya Nelson Mwakilasa na Felister Mwanisongole ambayo imetokana na shauri la jinai Na. 77/2023, imetolewa Machi 22,2024 chini ya Mhe. Mtengeti Sangiwa ambaye ni Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mbeya.

Mbele ya Mahakama ilidaiwa washtakiwa hao walishawishi kuomba na kupokea hongo ya Shilingi 75,000 kutoka kwa wafanyabiashara.

Lengo ni kuwaruhusu wafanyabiashara katika Soko la Magorofani ndani ya jiji la Mbeya, kufanya biashara bila ya kuwa na leseni ya biashara.

Aidha,washtakiwa wamelipa faini na kuachiwa huru na mahakama imewaamuru washtakiwa warejeshe kiasi cha shilingi 75,000 walichopokea toka kwa wafanyabiashara ili zirejeshewe kwa waathirika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news