Wauza mifugo wa Mnada wa Upili Tabora wahimizwa kufuata taratibu,wanaokiuka waonywa

NA ABEL PAUL
Tanpol

JESHI la Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo limesema litaendelea kutoa elimu kwa wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo hapa nchini.

Pia,limebainisha kuwa,halitomuonea muhali mfugaji yeyote atakayebainika kutorosha mifugo na kukiuka taratibu za uuzaji wa mifugo hapa nchini.
Hayo yamebainisha leo Machi 9, 2024 Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora na Kamanda wa Polisi kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo hapa nchini,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,SACP Simon Pasua.

Ni baada ya kutembelea mnada wa Upili Igunga ambapo amebainisha kuwa, kikosi hicho kitaendelea kutoa elimu kwa wafugaji nchi nzima ili kuondokana uvunjifu wa sheria.
SACP Pasua ameongeza kuwa wafugaji hapa nchini wanatakiwa kufuata taratibu za uuzaji wa mifugo yao ambapo amesema watakao kiuka taratibu hizo kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo kitaendelea kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani wale wote watakaobainika kuvunja sheria.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kote nchini kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi za baadhi ya watu wanaojihusisha na wizi wa mifugo ili hatua sitahiki zichukuliwe kwa watao bainika kujihusha na uhalifu huo hapa nchini.

Baadhi ya wafanyabiashara wa mifugo katika mnada wa Upili wa wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Pamoja na kushukuru jitihada za Jeshi la Polisi katika kutoa Elimu kwa wafugaji wameomba elimu zaidi itolewe kwa wafugaji ili kujenga uelewa wa Pamoja.
Naye Meneja wa Mnada wa Upili Igunga Mkoani Tabora,Yohana Mtende amesema hapo awali kulikuwepo na changamoto ya uzio wa kisasa katika mnada huo ambapo ameliomba Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo kuendelea kuimarisha Usalama wa Mifugo katika mnada huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news