Waziri Kairuki aongoza ujumbe wa Tanzania jijini Berlin

BELIIN-Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki katika ufunguzi wa Maonesho ya Utalii ya ITB yaliyofanyika Machi 4,2024 jijini Berlin, Ujerumani.
Katika hafla hiyo, Mhe. Kairuki kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maliasili na Utalii wa Oman, Mhe. Salem bin Mohammed Al Mahrouqi, Waziri wa Utalii wa Saudi Arabia, Mhe. Ahmed Al Khateeb, Naibu Waziri wa Utalii wa Saudi Arabia, Princess Haifa Al Saud pamoja viongozi mbalimbali wa Sekta ya Utalii Barani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news