Waziri Mkuu amwakilisha Rais Dkt.Samia maziko ya mke wa MNEC,Christopher Mwita Gachuma

MARA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Jana 30 Machi 2024 alimuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maziko ya Askofu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NLGCC ) Jimbo la Mara Kaskazini, Bi. Fransisca Mwita Gachuma ambaye pia ni mwenza wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (NEC), Christopher Mwita Gachuma.
Mheshimiwa Majaliwa alisema,Mheshimiwa Rais Samia suluhu Hassan ameguswa na msiba huo na ataendelea kuthamini na kutambua mchango mkubwa wa familia ya Gachuma kwa wananchi wa Tarime na Tanzania kwa ujumla.

Naye, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuyachukua mafunzo ya marehemu ili kujiimarisha zaidi na kukijenga chama hicho.
Maziko hayo yalifanyika katika Kijiji cha Komaswa Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news