Waziri Ulega ashiriki futari na wabunge

DAR ES SALAAM-Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiambatana na Watendaji wa Wizara yake ameshiriki futari na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo iliyoandaliwa na Wizara yake jijini Dar es Salaam Machi 18, 2024.
Tukio hilo la futari lilihudhuriwa pia na Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar na wananchi wengine.
Akizungumza baada ya tukio hilo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mhe. Mariam Ditopile alimpongeza Waziri Ulega na Watendaji wake kwa kuisimamia vizuri Wizara huku akiahidi kuwa Kamati hiyo itaendelea kutoa ushirikiano ikiwemo kuhakikisha bajeti ya wizara inaongezeka ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news