Waziri wa Fedha ateta na Mkurugenzi mpya wa TBL


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kushoto, akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Bi. Michelle Kilpin (kulia), kuhusu Kampuni yake kuendelea kuchangia maendeleo ya jamii, alipofika kujitambulisha, katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri (Treasury Square), jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza jambo wakati wa mkutano wake na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Bi. Michelle Kilpin (hayupo pichani), baada ya kufika kujitambulisha, ofisini kwake (Treasury Square), jijini Dodoma, ambapo amepongeza jitihada za Serikali za kuimarisha Sera zinazoweka mazingira bora ya ufanyaji biashara.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Bi. Michelle Kilpin, akizungumza kuhusu mchango wa Kampuni yake katika maendeleo ya uchumi, alipofika kujitambulisha kwa Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ofisini kwake (Treasury Square), jijini Dodoma.
Kamishna wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja, akifafanua jambo kuhusu Sera ya fedha wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Bi. Michelle Kilpin (hawapo pichani), kushoto kwake ni wajumbe wa mkutano huo kutoka Wizara ya Fedha, jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Sera wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls Kusini mwa Jangwa la Sahara, Bi. Mesiya Mwangoka, akiwasilisha hoja mbalimbali zinazohusu biashara ya Kampuni hiyo mbele ya Mhe. Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) alipoongozana na Mkurugenzi Mpya wa Kampuni hiyo, Bi. Michelle Kilpin (kulia), aliyefika kujitambulisha jijini Dodoma
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Bi. Michelle Kilpin, baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha (Treasury Square), jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha na kuelezea mipango ya Kampuni yake katika uzalishaji wa vinywaji pamoja na mchango wake katika maendeleo ya nchi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Michelle Kilpin (wa tatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Wizara ya Fedha na TBL baada ya kumalizika mkutano kati yao, katika Ukumbi wa Waziri wa Fedha (Treasury Square), jijini Dodoma ambapo wamejadili mchango wa Kampuni hiyo katika maendeleo ya nchi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Bi. Michelle Kilpin, baada ya kufika Ofisi za Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma, kujitambulisha, ambapo Mkurugenzi Mtendaji huyo ameipongeza Serikali kwa kuboresha mazingira ya kufanyabiashara na kuahidi kuwa Kampuni yake itaendelea kuchangia maendeleo ya nchi kupitia program mbalimbali za kusaidia jamii na kulipa kodi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news