Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungary awasili nchini kwa ziara ya kikazi

DAR ES SALAAM-Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary, Mhe. Péter Szijjártó amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili tarehe 27 na 28 Machi 2024.
Katika Uwanja wa Ndege wa JNIA amepokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Said Shaib Mussa.
Wengine walioshiriki katika mapokezi hayo ni Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Swahiba Mndeme; Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga; Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Gerald Mbwafu pamoja na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Hungary mwenye makazi yake nchini Ujerumani, Bi. Angela Ngailo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news