Wanakijiji waanza ujenzi David Massamba Memorial Secondary School

NA FRESHA KINASA

WAKAZI wa Kijiji cha Kurwaki, Kata ya Mugango Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara wameanza ujenzi wa David Massamba Memorial Secondary School." Wakishirikiana na Mbunge wa Jimbo hilo Prof. Sospeter Muhongo.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akiwa na wanakijiji wa Kurwaki kwenye eneo la ujenzi wa,David Massamba Memorial Secondary School hivi karibuni.

Prof. Muhongo ambaye ni mpenda maendeleo amechangia mchango wake binafsi wa mifuko 250 ya saruji, na mifuko 205 ya saruji kutoka nfuko wa jimbo hilo.

Hayo yamebainishwa leo Machi 27, 2024 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa la Musoma Vijijini.

''Sekondari hii ambayo itakuwa ya pili kwa Kata ya Mugango inajengwa ikiwa imepewa jina la marehemu Prof. David Massamba, mzaliwa wa Kijiji cha Kurwaki, na aliyekuwa bingwa wa mabingwa wa lugha ya Kiswahili. 

"Kazi kubwa za ustawishaji wa Lugha ya Kiswahili zilifanywa na Marehemu Prof. David Massamba, kwa kushirikiana na Wataalamu wenzake,"imeeleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa.
"Kazi hizo ni pamoja na kuandika vitabu vinavyotumika Vyuo Vikuu na Sekondari (Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu),Uandishi wa Kamusi ya Kiswahili."

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa michango ya awali ya ujenzi wanakijiji ni shilingi 1,870,000,
familia Massamba shilingi 800,000,

Wazaliwa wa wa Kurwaki Shilingi 750,000 Dr Rukonge Manoko & Kawawa Jackson), Diwani wa Kata shilingi 200,000, Wazazi wa Kijiji jirani, Kiriba shilingi 80,000.
Wengine ni walimu makada shilingi 70,000.Huku Akaunti ya Kijiji ya kutuma michango ni Benki: NMB;
Akaunti Na: 30302301539
Jina: Kijiji cha Kurwaki.
"Tafadhali tunaomba tuendelee kuchangia ujenzi wa Sekondari hii ambayo itakuwa ni kumbukumbu nzuri ya kuenzi kazi nyingi na muhimu sana alizozifanya Marehemu Prof. David Massamba kwenye ukuzaji na usitawishaji wa Lugha ya Kiswahili kitaifa na kimataifa,"imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news