Zuchu afungiwa miezi sita Zanzibar

ZANZIBAR-Baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la Zanzibar, ( BASSFU), limemfungia msanii wa kizazi kipya Zuhura Othman Masoud maarufu kwa jina la Zuchu kuendesha shughuli zote za sanaa visiwani Zanzibar kwa kipindi cha miezi sita.
BASSFU pia limepiga marufuku redio na televisheni za visiwani humo kupiga nyimbo zake zote kwa kipindi hicho.

Hatua hiyo imekuja baada ya tukio la hivi karibuni Zuchu akiwa jukwaani kwenye Tamasha la Full Moon Party akitumbuiza na alitoa matamshi na kuonesha ishara mbaya ambazo ni kinyume na maadili ya Kinzanzibari.

Pia,alijitapa kwa madaha stejini kwa kuimba kuwa wanawake wote wanaomwendea mwanaume wake kamwe hawawezi kumtoa mikononi mwake hata wakimpa kinyume na maumbile huku akionesha kwa ishara.
Hata hivyo, baada ya tamko hilo, Zuchu ameandika barua ya kuomba radhi kwa BASSFU pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) huku akielezea kuwa nia yake ilikuwa njema ya kutaka kutoa burudani na furaha kwa mashabiki wake.

Najua kuwa maneno yalileta sintofahamu kwa wengi wenu na kuleta maana hasi kwa jamii na mashabiki zangu kwa ujumla, nia yangu ilikuwa ni kuleta burudani njema na furaha kwa mashabiki wangu wote."

Zuchu amesema halikuwa lengo lake kupotosha, kumong’onyoa maadili au kuleta taharuki, hata hivyo Zuchu ameahidi kufanya kazi na timu yake ili kuhakikisha matukio kama hayo hatokei tena.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news