Al Ahly yawatoa Simba SC michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika

CAIRO-Klabu ya Al Ahly ya nchini Misri imezima ndoto ya Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa barani Afrika.
Ni kupitia mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly uliopigwa usiku wa kuamkia Aprili 6,2024 Uwanja wa Cairo International ambapo umemalizika kwa kupoteza kwa mabao 2-0.

Simba SC walianza mchezo kwa kasi huku wakishambulia lango la Al Ahly, lakini walipoteza nafasi kadhaa walizotengeneza.

Amr El Soulia aliwapatia wenyeji Al Ahly bao la kwanza dakika ya 47 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Anthony Modeste.

Baada ya bao hilo,Simba SC waliongeza kasi ya kutafuta bao la kusawazisha na kuongeza nyingine,lakini wenyeji Al Ahly walikuwa imara zaidi.

Al Ahly walipata bao la pili dakika ya mwisho ya mchezo kupitia kwa Mahmoud Kahraba baada ya mlinzi Che Malone kumchezea madhambi Hussein El Shahat ndani ya 18.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news