Anayedaiwa deni Kariakoo mpya ataiona na kuisikia tu, Mfumo wa TAUSI kutumika

DAR ES SALAAM-Shirika la Masoko ya Kariakoo (KMC) limewataarifu wafanyabiashara na wananchi kuwa kutokana na maboresho yanayofanyika katika uendeshaji wa biashara katika soko jipya la Kariakoo na maagizo ya Serikali kutumia mifumo ya kielektoniki ili kuleta tija, shirika litatumia mfumo wa kielektoniki wa TAUSI kutangaza maeneo ya biashara na kukusanya mapato.
Picha zikionesha majengo ya soko jipya la Kariakoo ambalo kwa sasa limefikia asilimia 93 ya ujenzi na ukarabati na linatarajiwa kukamilika na kuanza kazi hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Kaimu Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, Bw. Sigsibert K.Valentine amesema, shirika halitaruhusu mfanyabiashara mwenye deni la awali kupata umiliki wa eneo la kufanya biashara katika Soko la Kariakoo.

Valentine amewataka wafanyabiashara wote wanaodaiwa kulipa madeni yao kabla ya kuomba tena nafasi ya kurejea kwenye maeneo yao ya biashara.
Kaimu Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bw. Sigsibert K.Valentine akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam (22 Aprili 2024) kuhusu maandalizi ya wafanyabiashara kurejea sokoni Kariakoo ambapo amesema mfanyabiashara mwenye deni la awali anapaswa kulipa kabla ya kuomba nafasi tena kwa kuwa mfumo wa kielektoniki utakaotumika hautoruhusu wadaiwa kuingia soko jipya la Kariakoo.

“Shirika la Masoko ya Kariakoo linadai jumla ya Shilingi 497,773,019.26 ambazo ni madeni yaliyolimbikizwa kwa muda mrefu.

"Madeni haya yanapaswa kuwa yamelipwa na wafanyabiashara kabla ya kurejea sokoni ili wapate nafasi ya kusajiliwa kwenye mfumo,” alisisitiza Valentine.
Kaimu Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo Bw. Sigsibert K.Valentine akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam (22 Aprili 2024) kuhusu maandalizi ya wafanyabiashara kurejea sokoni Kariakoo ambapo amesema mfanyabiashara mwenye deni la awali anapaswa kulipa kabla ya kuomba nafasi tena kwa kuwa mfumo wa kielektoniki utakaotumika hautoruhusu wadaiwa kuingia soko jipya la Kariakoo.

Katika hatua nyingine,Kaimu Meneja Mkuu huyo amemshurukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa shilingi Bilioni 28.03 zilizotumika kufanikisha mradi wa ujenzi na ukarabati wa soko la Kariakoo ambao kwa sasa umefikia asilimia 93.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news