Dkt.Biteko awasili Pemba

ZANZIBAR-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili Kisiwani Pemba na kupokelewa na Waziri ofisi ya Makamo wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la wawakilishi Mhe. Hamza Hassan Juma kwa ajili ya shughuli za maandalizi ya maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofikia kilele chake terehe 26 April 2024.
Akiwa Kisiwani humu Dkt. Biteko ataweka jiwe la Msingi wa Ujenzi wa kituo cha Afya, Shehia ya kinyikani Jimbo la Kojani Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news