Elimu,OR-TAMISEMI kuja na mikakati wanafunzi shule zilizokumbwa na mafuriko kuendelea na masomo

DODOMA-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,Prof.Adolf Mkenda amesema, Serikali itahakikisha inaweka mazingira ya wanafunzi wote ambao shule zao zimeathirika na mafuriko nchini kuendelea na masomo.
Amesema hayo Aprili 15, 2024 jijini Dodoma katika kikao kati ya Uongozi wa wizara hiyo na Ofisi ya Rais - TAMISEMI kilichokuwa na lengo la kujadili mikakati ya utekelezaji wa Mageuzi ya Elimu kulingana na Sera ya Elimu na Mafunzo na Mitaala iliyoboreshwa na kuongozwa na mawaziri wa wizara hizo.
"Tumekutana kwa ajili ya utekelezaji sera,lakini kubwa lililo mbele yetu kwa sasa ni kuhakikisha tunawezesha wanafunzi waliokwama kuendelea na masomo kutokana na athari za mafuriko nchini wanawezeshwa kuendelea na hii ni kwa shule zote za serikali na binafsi," amesema Prof. Mkenda.Mawaziri hao wameagiza wataalamu kupata taarifa za tathmini kutoka kwa Wathibiti Ubora na Maafisa Elimu walio katika maeneo mbalimbali nchini na maeneo mengine waweze kufika na kuja na mipango ya muda mfupi na mrefu ya kutekeleza agizo hilo ikiwemo upatikanaji rasilimali.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa OR-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema, wataalamu wanapaswa kuandaa maandiko ya upatikanaji fedha kutoka kwa washirika wa maendeleo ambao wako tayari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news