Gavana Tutuba ateta na ujumbe kutoka Shirika la MCC

DAR ES SALAAM-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Emmanuel Tutuba amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Shirika la Millenium Challenge (MCC) ukiongozwa na Bw. Bradley Cunningham na kujadili mambo mbalimbali kuhusu upatikanaji wa huduma za fedha nchini na uwepo wa mazingira rafiki ya uwekezaji na biashara ambayo ni nyenzo muhimu katika ustawi wa sekta ya fedha.
Kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za Makao Makuu Ndogo ya BoT, Dar es Salaam, kilihudhuriwa pia na Naibu Gavana (Sera za Uchumi na Fedha), Dkt. Yamungu Kayandabila, na maafisa wengine waandamizi wa BoT.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news