Matapeli wanaojitambulisha ni MO Dewji Mikopo huko Facebook wakanyaga pabaya

DODOMA-Kumekuwa na taarifa inayosambaa mitandaoni kupitia ukurasa wa facebook wenye jina la MO DEWJI MIKOPO ikiambatishwa na maneno yaliyochapishwa kwenye video hiyo kusisitiza imani ya Mhe. Waziri Mkuu na taasisi hiyo.
Kwa taarifa hii, tunapenda kuujulisha umma kuwa, Mheshimiwa Waziri Mkuu alizungumza maneno hayo katika uzinduzi wa Program ya IMBEJU iliyolenga kuwawezesha vijana kiuchumi ambayo inadhaminiwa na benki ya CRDB, uzinduzi huo ulifanyika Machi 12, 2023 Jijini Dar es Salaam na wala hakuzungumza lolote kuhusu taasisi tajwa kwenye ukurasa huo.

Ofisi ya Waziri Mkuu inautaarifu umma kuwa Serikali inatambua na kuthamini taasisi mbalimbali zinazotoa mikopo kwa makundi mbalimbali kupitia taratibu rasmi walizojiwekea.

Aidha, Ofisi inautaarifu umma kuwa Serikali inao utaratibu wa utoaji mikopo kwa wananchi kupitia Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Hivyo wananchi wanao hitaji kupata taarifa za mikopo ni vyema kufika katika Idara za Maendeleo ya Jamii zilizopo katika Halmashauri zote nchini pamoja na Ofisi za Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi.

Kupitia Taarifa hii, Ofisi inatoa onyo kwa wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kuzusha kwa kuchapisha zisizo na ukweli kwa kuwahusisha viongozi wa Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news