Mheshimwa Byabato awagawia wananchi Kisiwa cha Musira kadi za bima ya afya

KAGERA-Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Mhe. Stephen Byabato amegawa kadi 18 za Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa kwa watu wa makundi maalum Kisiwani Musira kilichopo Kata ya Miembeni Jimbo la Bukoba Mjini mkoani Kagera.
Byabato amesema zoezi hilo ni endelevu ambapo watu wa Makundi Maalum wakiwemo Walemavu na Wazee takribani 140 katika kata zote za Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wanatarajia kupata bima ili kuwasaidia kupata huduma za afya kwa urahisi kwenye vituo vya Serikali pale watakapokuwa na uhitaji wa huduma hiyo.
Ameongeza kuwa kadi za Bima ya Afya zitatolewa kwa wananchi kumi kutoka kila kata ndani ya jimbo hilo.

Wananchi wa Kisiwa cha Musira waliopata bima hizo wamemshukuru Mbunge Byabato kwa kuwapa msaada huo na kukiri kuwa bima hiyo ni mkombozi kwao katika kupata huduma stahiki za afya.

Wamesema wakati mwingine walikuwa wanapata changamoto ya kupata huduma za afya kwa kuwa walikuwa hawana fedha hivyo Bima hizo zitawasaidi sana.

Awali, Bi. Juleth Richard, akisoma risala iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Musira, amesema kuwa katika mtaa huo yapo mambo mengi ambayo yamefanyika ikiwa ni pamoja na ujenzi wa choo, Boti ya Mv Byabato na majiko ya gesi kwa mama na Baba lishe.
Baada ya kufika kisiwani hapo Mbunge Byabato akiwa ameambatana na kamati ya maandalizi ya shughuli hiyo, wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka Jimbo la Bukoba Mjini na wajumbe kutoka group la Whatsapp la Bukoba Mjini Mpya walifanya shughuli mbalimbali ikiwemo kupanda miti kwa ajili ya kutunza mazingira.
Pia,uzinduzi wa Boti ya Mv Byabato, uzinduzi Choo cha matundu 4, ugawaji wa Mipira minne kwa ajili ya Timu ya mpira ya Musira na kutoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya mikopo ya kopa kwa mbunge lipa kwa mwingine na usimikwaji wa Taa zenye mwanga safi pale mwaloni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news