Morogoro yajipanga kuhamasisha matumizi ya mbolea

MOROGORO-Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa Ally Mussa ameahidi kuwa mkoa wake utashiriki kikamilifu katika kuhamasisha matumizi ya mbolea na kusaidia kuondoa imani potofu kuwa udongo wanaoulima una rutuba ya kutosha na kusababisha matumizi hafifu ya mbolea.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Anthony Diallo akizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ally Mussa katika kikao kifupi cha kuhamasisha matumizi ya mbolea mkoani humo tarehe 22 Aprili, 2024.

Amesema wakulima wengi wanaamini udongo wao unarutuba kutokana na kupokea rutuba inayosafirishwa kutoka milimani wakati wa mvua kubwa.Wakala wa mbolea wa kampuni la Okota Agrovert Ltd, Mendrad .J.Okota akiwasilisha hoja kwa Bodi na Menejimenti ya TFRA wakati wa kikao baina ya TFRA na Wafanyabiashara wa mbolea wa Mkoa wa Morogoro kilichofanyika katika ukumbi wa TARI ndani ya viwanja vya maonesho ya Nanenane mkoani Morogoro tarehe 22 Aprili, 2024.

Dkt. Mussa amesema hayo tarehe 22 Aprili, 2024 alipokuwa akizungumza na Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ilipofanya ziara ofisini kwake iliyolenga kuhamasisha Ofisi za Mkoa kushiriki katika kuhamasisha matumizi ya mbolea pamoja na kupima afya ya udongo ya watu wake kupitia vifaa vilivyogawiwa na Wizara kwa Maafisa Ugani wa Kata zote nchini.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro akizingumza na Bodi na Menejimenti ya TFRA (hawapo pichani) walipomtembelea ofisini kwake kuhamasisha ushiriki wa Mkoa kwenye kuhamasisha matumizi ya mbolea kwa wakulima wa mkoa huo tarehe 22 Aprili, 2024.

Changamoto nyingine ni uelewa mdogo wa matumizi sahihi ya mbolea na jiografia ya mkoa ni suala jingine linalosababisha matumizi hayo kuwa hafifu.

Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo aliiomba Ofisi ya Mkoa kuhimiza maafisa ugani ndani ya mkoa huo kupima afya ya udongo na kuwasilisha taarifa za upimaji huo ili kuwasaidia wakulima kujua aina ya mbolea wanayopaswa kutumia kulingana na mahitaji ya udongo na hivyo kuongeza tija.Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ally Mussa kulia akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya TFRA, Dkt. Anthony Diallo katika kikao kilichofanyika ofisini kwake tarehe 22 Aprili, 2024.

Aidha, ameomba uongozi wa mkoa huo kuwashirikisha wafanyabiashara wa mbolea kwenye vikao vya pembejeo ili wapate maoni yao kabla ya kuwasilisha TFRA ili yazingatiwe wakati wa kupanga bei elekezi na hivyo zilingane na umbali wa maeneo wanakofikisha bidhaa hiyo.Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) akizungumza na wafanyabiashara wa mbolea juu ya wajibu wao wa kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima wa Mkoa wa Morogoro ili waweze kuongeza tija katika kikao baina yao kilichofanyika tarehe 22 Aprili, 2024.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA, Joel Laurent ameuomba uongozi wa Mkoa kuhimiza wananchi wake kujisajili ili waweze kunufaika na ruzuku ya mbolea inayotolewa na serikali ili kuwapa ahueni ya gharama za uzalishaji wakulima.

Amesema mpaka kufikia tarehe 14 Aprili, 2024 jumla ya wakulima 138,538 wamesajiliwa kwenye mfumo wa mbolea za ruzuku na wanufaika wa mpango huo ni wakulima 13,653 walionunua kiasi cha tani10,808.15 za mbolea.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Mbolea Tanzania, Gerold Mlenge akizungumza wakati wa kikao baina ya Bodi, Menejimenti ya TFRA na Wafanyabiashara wa mbolea wa Mkoa wa Morogoro tarehe 22 Aprili, 2024.

Akiwasilisha ombi la wafanyabiashara wa mbolea katika kikao baina yao na TFRA Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara wa Mbolea, Gerold Mlenge aliiomba Mamlaka kupanga bei elekezi kulingana na umbali halisi wa maeneo inakopaswa kufika kwani maeneo mengi ya mkoa huo yako mbali na makao makuu ya wilaya ili waone faida ya kufanya biashara hiyo na wakulima wafikishiwe bidhaa hiyo karibu na maeneo yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news